Siku ya wapendanao au Valentine's day ina historia
ndefu sana. Nifahamishe tunawaletea historia ya siku hiyo kwa mujibu wa vyanzo
kadhaa vya historia ya siku hiyo.
Asili ya siku ya wapendanao "Valentine's
Day" ni St Valentine, mhubiri wa kikristo aliyekuwa akiishi karibu na mji
wa Roma katika karne ya tatu wakati wa utawala wa Claudis II.
Claudis alitaka awe na jeshi kubwa akategemea vijana
wangejitolea na kujiunga na jeshi lake.
Lakini vijana wengi hawakupenda vita kwakuwa
hawakutaka kuziacha familia zao na watoto wao.
Claudis akafikiria akaona hawa vijana kuwakomesha
waingie jeshini ni kupiga marufuku watu kuoana.Kuanzia hapo akapiga marufuku
watu kuoana akitegemea vijana hawatajali sasa kujiunga na jeshi kwasababu ya
familia zao.
Askofu Valentine naye kwa siri akawa anawafungisha
ndoa vijana hao kwa siri.
Claudius aliposikia habari hizo aliamuru Valentine
akamatwe na akahukumiwa adhabu ya kifo cha kunyongwa.
Wakati akiwa jela akisubiri siku yake ya kunyongwa
Valentine alikuwa akitembelewa na vijana waliokuwa wakimpelekea maua kuonyesha
wako pamoja nae.
Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda kumtembelea ni
mtoto wa mkuu wa gereza ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka kwenye selo la
Valentine "kupiga naye stori".
Inasemekana kwamba Valentine aliangukia katika mapenzi
na binti huyo wa mkuu wa gereza wakati anasubiria kunyongwa.
Inasemekana kwamba muda mchache kabla hajanyongwa
Valentine aliomba kalamu na karatasi na kuandika meseji yake ya kuaga akiweka
sahihi "From Your Valentine" ( kutoka kwa Valentine wako )
Valentine akanyongwa tarehe 14 februari mwaka 269 AD.
Baada ya kunyongwa kwa Valentine, vijana wa Roma
walianza kumuiga Valentine na kuwaandikia na kuwatumia wanawake waliowapenda
salamu za mapenzi.
Tangia siku hiyo tarehe hiyo ikaanza kuhusishwa
urafiki, upendo na mahaba duniani huku ikihusishwa zaidi na mambo ya mapenzi.
Siku hiyo imezidi kuwa maarufu kila miaka inavyoenda
huku huku makampuni yakiigeuza siku hiyo kuwa ya biashara zaidi kwa kufanya
kila kitu maalumu kwa siku ya wapendanao kionekane kuwa inabidi kiwe chekundu
kuanzia kadi za salamu, maua, mpaka nguo wavaazo wapendanao inabidi ziwe
nyekundu.
Kuna watu wengi pia ambao hawasherehekei siku hii kwa
kuhoji umuhimu wa kuonyesha kumjali umpendaye katika siku moja tu ya mwaka
badala ya siku zote 365.
Post a Comment