
Hizi ni njia tatu
zinazoweza kusaidia mahusiano yako kudumu kwa muda mrefu:
Geuza mtazamo wa mapenzi
Unapaswa kutumia kila
nafasi unayoipata kufanya mapenzi kama nafasi ya kumuonyesha kitu kipya mpenzi
wake – Mwisho utagundua kitu kutoka kwa mpenzi wako huyo!
Jitahidi kusoma na
kujifunza njia mpya kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako hali itakayopelekea
kumlinda mpenzi wako asitoke nje ya mahusiano yenu.
Watu wengi wamezoea kuwa
mwanaume ndio kiongozi wa kila kitu, hali iliyopelekea mpaka wanawake wengi
hawezi kumuambia mtu wake kuhusu kufanya ‘tendo’ mpaka mwanaume ndio aanze
kusema. Hilo kwenye mapenzi ni kitu ambacho kinapaswa kuwekwa kando ili kuleta
furaha kwenye mapenzi yenu.
Tafuta ushauri
Kuna mbinu nyingi ambazo
wapenzi hudhani wanazijua, lakini ni njia moja ya kuhakikisha kuwa mapenzi
yananoga kila siku ni kutafuta mbinu mpya na za kipekee.
Wapenzi wengi wamekuwa
waoga kuomba ushauri kama kuna matatizo ndani ya mahusiano yao, hali
inayopelekea mtu huvumilia matatizo hayo mpaka mwisho wake huamua kulisaliti
penzi lake kwa kutafuta furaha kwa mtu mwingine.
Kwenye mapenzi siyo kila
rafiki wala mtu wako wa karibu anaweza kukupa ushauri mzuri utakaokufaa – Kuna
wengine watakushauri vibaya ukajutia maamuzi yako hapo mbeleni. Unaweza
kuwafuata watu waliodumu kwenye mahusiano kwa muda mrefu wakiwa na furaha na
kuweza kuomba ushauri kujua wamefanyaje mpaka kufikia hapo ili uweze kufikia
malengo na mpenzi wako.
Tambua vitu
anavyovipenda/ havipendi mpenzi wako
Unapaswa kuvijua vitu
ambavyo havipendi mpenzi wako ili kujiepusha na kumkwaza mara kwa mara ili hata
ikitokea hivyo ujue kwa wakati huo yupo kwenye ‘mood’ gani.
Post a Comment