Mahitaji
ü Mchele nusu kilo , Uliosafishwa kwa maji
ü Viazi nusu kilo – menya, na uvisafishe kwa
maji
ü Nyama Nusu kilo, Kuku au nyama ya samaki.
ü Kikombe kimoja cha mafuta ya alizeti (au
mafuta yeyote ya kula)
ü Vikome 4 vya maji ya moto au Supu
ü Kitunguu 1, kilicho menywa
ü Vijiko 5 vya karafuu iliyosagwa
ü Tangawizi iliyosagwa (kijiko 1 au 2)
ü Nyanya 2, zilizokatwa katika vipande
vidogovidogo
ü Viungo vya Pilau Vijiko 2 (Vilivyosagwa)
ü Chumvi na Pilipili kwa ajili ya Kuongeza ladha
nzuri
Maelekezo
Chemsha nyama pamoja na tangawizi kwa dakika
10. Weka Viazi na uache vichemke kwa dakika tano na epua uweke pembeni
(tenganusha supu hivyo unaweza kutumia baadaye)
Pasha mafuta na weka vitunguu hadi
vibadilike rangi na kuwa brown, weka vitunguu na Viungo vya pilau na changanya
kwa dakika 1, kwa moto mdogo.
Weka nyanya, nyama pamoja na viazi na Koroga
Weka mchele na hakikisha mchanganyiko wa kila
kitu umechanganyika vizuri kabla ya kuweka supu au maji ya moto, na koroga
vizuri.
Weka chumvi na pilipili kwa ajili ya Kuongeza
ladha, alafu funikia chakula chako kiive kwa moto wa kawaida
Chakula chako kikianza kukaukia, Punguzia moto
kwa chini, na Funikia Pilau yako, na iache iive kwa dakika 10
Hapo pilau yako itakuwa tayari!
"Kama una maoni, ushauri, na mapendekezo kuhusu chapisho hili, usisite kutuandikia maoni yako
katika kisanduku cha maoni hapa chini nasi tutayafanyia kazi."
Post a Comment